KOCHA BARCELONA (ERNESTO VALVERDE) AONGEZEWA MKATABA MPYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 15, 2019

KOCHA BARCELONA (ERNESTO VALVERDE) AONGEZEWA MKATABA MPYA

Fc Barcelona

Kocha wa klabu ya FC BARCELONA ya nchini Hispania, Ernesto Valverde amekubali kuongeza mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha wakatalunya hao mpaka mwisho wa msimu ujao (2019/2010) huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi pia. 

Valverde amesaini mkataba huo rasmi leo IJUMAA na kuzinyamazisha tetesi za kuondoka kwake mwisho wa msimu huu ambazo zilikuwa zimezagaa sana mitaani na mitandaoni. 

Valverde alichukua nafasi ya Luis Enrique mwaka 2017 na kuwa kocha wa klabu hiyo ambapo ameiongoza kuchukua kombe la ligi pamoja na la mfalme katika msimu wake wa kwanza kama kocha mkuu. 

Klabu hiyo ya FC BARCELONA wapo kileleni mwa Ligi yao maarufu kama LALIGA wakiongoza kwa tofauti ya pointi 6 na wapinzani wao wakuu REAL MADRID huku zikiwa zimebakia mechi 15 kuchezwa za msimu huu. 

Pia wapo katika hatua ya mtoano katika ligi ya mabingwa Ulaya na watacheza wiki ijayo dhidi ya Olympic Lyon ya Ufaransa. 


Loading...

No comments: