#KUELEKEA VALENTINE;NO LOVE WITHOUT TRUST...JINSI YA KURUDISHA IMANI ILIYOPOTEA KWA MPENZI WAKO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 11, 2019

#KUELEKEA VALENTINE;NO LOVE WITHOUT TRUST...JINSI YA KURUDISHA IMANI ILIYOPOTEA KWA MPENZI WAKO

No Trust No Love..


Penzi bila Kuaminiana ni sawa na Kuku asiye na Firigisi,bei rahisi sana aisee...

And when the trust is lost,si rahisi kuirudisha...Relationship nyingi zilizoishiwa Trust hufa kibudu,chache sana zimeweza kuibuka tena baada ya kazi ngumu na shughuli pevu sana.


Kuna sababu nyingi sana huua Trust among Lovers...Wengine wamefumania Wapenzi wao red-handed kitandani au gheto anauza Share bila ruhusa ya Menejimenti...Wakakosa pozi,wakalia,wakadhani wamesamehe lakini inawauma sana,kila wakikumbuka kile kitendo wanahisi things will never come back to normal...


Wengine wamekuta Meseji kutoka kwa Wanaume/Wanawake wengine kwenye Simu za wapenzi wao,ikawaua nguvu....Hakuna Cheating rahisi,na Wameshindwa kuwaamini tena no matter how many months have passed....


Inataka moyo sana kujikakamua na kurudi Mwanzoooo...Kama hakuna kilichotokea,wengi hawawezagi kurudi pale....Inataka Moyo! Wengine wanajikuta wanalipiza kwa kutafuta kidumu,kama alifanya basi atafanya tena,aah ngoja na mimi nitafute cha kwangu ili twende sawa...KOSA! Akigundua,there will never be a relation, it will die completely


FANYA HAYA KURUDISHA TRUST ILIYOPOTEA

1.Admit

Ukikumbana na kimeo,hakuna kujifanya wewe mjuaji,ADMIT kosa..Kama akiamua kukusamehe,asamehe,akiamua kukuacha akuache....Ukijifanya kidume kukataa kosa kumbe mwenzio anajua kila kilichotokea,atakaa kimya na atakulipizia in a place hutaamini. Hakuna ujanja kwenye hili,if you are in love with that person,show that ur regreting and you need to change!

Ubishi unaonyesha kwamba ulichofanya ni kawaida,na kwako sio kosa na haikuumi,and thats bad

2.Be Open and Honest

Baada ya kimeo kutokea,umeshaadmit you were wrong...Kifuatacho ni kumuonyesha kwamba kweli umedhamiria kutokurudia kosa

Ule uwazi ambao mwanzo haukuwepo,hapa ndio mahala pake....Kuwa muwazi,usiwe na hidden issues,hidden agendas ambazo kwa namna moja au nyingine ita-trigger Mawazo kwamba kuna mambo bado unafanya kwa siri.

Ratiba zako ziwe wazi,wapi ulipo,unafanya nini...Na usisubiri kuulizwa ukipo,ifanye iwe daily habit,ukizoea utaona rahisi,ukisubiri uulizwe utahisi uko Misri utumwani

Mfanye akuone wa tofauti kwa kuwa muwazi...Itamsaidia kupona na kusahau lililotokea.Ukijifanya Hero kuendelea kuficha,kile kidonda hakitapona!

3.Act Differently to heal Him/Her
Kila kilichokuwa kikwazo mwanzo jaribu kukirekebisha.Haina ujanja,ndo ushaharibu,lazima ufanye kazi kubwa sana kurudisha upya....Na usihisi kama ni mzigo maana umejitafutia,umejenga na ukabomoa mwenyewe,so ni kazi yako kujenga tena.

Mtoe out kadri uwezavyo,Talk openly,Mshirikishe ratiba zako,Plan zako na kila kitu,ajihisi upya na kwamba sasa ur TOGETHER....Mfanye akuone mpya this time.

Ukifanya haya,ni kweli itachukua muda maana TRUST iliyopotea ni ngumu sana kurudi maana shetani ni yuleyule,kabadilika manyoya tu...Ni ngumu ila ukiinvest enough time and energy utaweza lasivyo be ready for a Bye Bye Kiss!
Loading...

No comments: