KUNA UWEZEKANO ALEXIS SANCHEZ ANAWEZA KUONDOKA MAN UTD, AKARUDI ARSENAL - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 15, 2019

KUNA UWEZEKANO ALEXIS SANCHEZ ANAWEZA KUONDOKA MAN UTD, AKARUDI ARSENALMshambuliaji wa klabu ya Manchester United anayehangaika kurudi katika kiwango chake, Alexis Sanchez anaweza kurudi klabu yake ya zamani ya Arsenal kulingana na alichosema kiungo wa zamani wa Arsenal Marc Overmars. 

Sanchez alijiunga na Mashetani wekundu mwezi Januari mwaka 2018 katika uhamisho uliomuhusisha winga Henrikh Mkhitaryan na amekuwa akihangaika kurudi katika kiwango chake kwa muda mrefu sasa. 

Mchile huyo wa miaka 30 sasa, amefunga magoli 5 tu katika mechi 37 alizocheza Manchester United na pia amekuwa akiandamwa na majeruhi mara kwa mara. 

Overmars ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Ajax ambaye anahusishwa na kuja kuhamia Arsenal katika nafasi hiyohiyo anaona kuwa Alexis anajuta kuondoka Arsenal kwa sasa. Overmars aliyaongea haya akiwa anahojiwa na radio ya Chile. 

Loading...

No comments: