Kutumia nguvu ya teknologia ya simu, kuongeza thamani ya jamii na uchumi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 7, 2019

Kutumia nguvu ya teknologia ya simu, kuongeza thamani ya jamii na uchumi


Miaka 50 iliyopita magari yalikuwa yakifanya kazi kutumia funguo, na baadae zikaja rimoti, mwaka 2020 mfumo wa compyuta unaojitegemea utawezesha magari kujiendesha kutumia mtandao wa 5G. Cha kustaajabisha zaidi miaka 50 iliyopita mtu wa kwanza alienda mwezini na sasa kampuni binafsi itapeleka roketi za kwanza zilizowezeshwa na teknologia ya 4G ambayo itafanya vitu vya duniani kuonyesha kwa mara ya kwanza picha za HD za mwezi.  Katika nyakati za sasa kampuni nyingi zimewekeza katika kuongeza thamani kwenye uchumi wa kidigitali, ambapo ubunifu wa mfumo wa kompyuta unaojitegemea umebadilisha jinsi watu wanavoishi na kuanya kazi. Mambo ambayo tulikuwa tunayaona kwenye filamu yamekuwa moja ya mambo katika jamii zetu

Ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inasema, Tanzania itakuwa na midomo milioni 77.5 ya kulisha na angalau vijana milioni 37 wa kuelimisha ifikapo mwaka 2030. Kilimo kinaendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, na kinaajiri asilimia 85 ya nguvu kazi, ambapo wakulima wadogo wadogo wanachukua asilimia 75 ya mazalisho yote katika sekta ya kilimo nchini, ambao ndio wenye idadi kubwa ya mazalisho kwa asilimia 85 ya mazao ya chakula katika heka 5.1, zinazo zalishwa na wakulima wadogo wadogo.
Na kadri idadi ya watu inavoongezeka ndivyo umuhimu wa serikali kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu bure kwa watanzania ili kuleta maendeleo unaongezeka. Sera ya elimu bure nchini imekuwa na mafanikio chanya katika kuongeza upatikanaji wa elimu. Mwaka 2007, Tanzania ilikaribia mafanikio ya upatikanaji wa elimu ya msingi kwa watu wote, ambapo uandikishaji ulifikia asilimia 97%. Ingawa tangia hapo undikishwaji wa watoto mashuleni umeshuka kutokana na changamoto mbali mbali hasa, usawa na viwango. Taarifa kutoka UNICEF inasema kuna pengo kubwa la upatikanaji wa elimu hasa kwa watoto wanaotoka katika familia masikini ambalo ni mara tatu zaidi ya wale wanaotoka katika familia tajiri. Nchini shule nyingi za vijijini zinaachwa bila uwekezaji wa miundominu muhimu ambayo ndio changamoto kubwa katika utoaJi wa elimu bora.
Makampuni ya mitandao ya simu yana nafasi ya kipekee kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi nchini. Kwani tunaona ubunifu mbali mbali katika kuboresha maisha ya kila siku kutoka kwenye bidhaa za simu kuanzia; elimu, afya na kilimo. Ripoti ya TCRA inaonyesha kuna zaidi ya milioni 40 ya watumiaji wa simu nchini Tanzania na kiwango cha upenyo asilimia 78. Simu inaweza kutumika kufungua matatizo yakila siku wakulima wadogo wadogo wanayokumbana nayo, kama, upatikanaji wa masoko na utunzaji wa taarifa. Kupitia mfumo wa Vodacom wa ‘Connected farmer’, unaotumia simu kusaidi biashara za kilimo na kuwawezesha wakulima kutumia M-Pesa kulipa na kupokea pesa na makampuni mengine. Huduma hii pia inasaidia uandikishaji na ukusanyaji wa taarifa muhimu kama matarajio ya mavuno ambayo inasaidia wasindikaji kupanga kitu ambacho kimepelekea upunguzaji wa gharama za uendeshaji.
Hivyo Hivyo kwa kushirikiana na serikali kuna nafasi kubwa ya kutegemea technologia kubadilisha sekta ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu bora. Ukiangalia teknologia za elimu zilizopo kuna haja ya kutia nguvu jitihada hizi zinazofanywa na watu mbali mbali. Ubunifu huu katika sekta ya kilimo na elimu ni mifano dhahiri kwamba teknologia ina changia kuleta maendeleo ya jamii. Teknologia ya simu kweli inanguvu ya kuhamasisha na kuleta mabadiliko hasi ambayo yanaleta mafanikio ya kiuchumi na kidigitali. Mwaka 2030 utakapo piga hodi hakuna mtu atabaki nyuma na watanzania watakaokuwa milioni 77 watajivunia maisha bora.


Loading...

No comments: