LEBRON JAMES YUPO TAYARI KUIONGOZA LAKERS KUFIKIA HATUA YA MTOANO MSIMU HUU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 21, 2019

LEBRON JAMES YUPO TAYARI KUIONGOZA LAKERS KUFIKIA HATUA YA MTOANO MSIMU HUU

LAKERS

Mchezaji wa timu ya Los Angeles LAKERS inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani, Lebron James amesema yupo tayari kupambana kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa timu yake inafika hatua ya mtoano katika ligi hiyo. 

Lebron ambaye amefikia hatua ya mtoano mara 13 mfululizo na timu tofauti na kufanikiwa kucheza fainali 8 mfululizo, aliandamwa na majeraha wiki chache zilizopita na kukosa michezo kadhaa ya Lakers ambayo mingi waliipoteza. 

Ikiwa imebaki michezo 25 katika msimu wa kawaida kabla ya hatua ya mtoano kufika, Lakers wameshinda mechi 28 na kupoteza michezo 29. Mwenendo huo umewafanya wawe katika nafasi ya 10 katika msimamo wa upande wa Magharibi. 

LAKERS

Lakers wapo nyuma ya Los Angeles Clippers kwa michezo 3 ambao wapo nafasi ya nane, pia wapo nyuma michezo 2 dhidi ya Sacramento ambao wapo nafasi ya 9. 

"SItakiwi kuwa comfortable kabisa," James alisema. "Napenda kutokuwa comfortable na jambo hili ni kati ya mengi yanayonifanya nisiwe comfortable na nalipenda".

James aliongezea kwa kusema kuwa mwaka huu "utakuwa wa tofauti kidogo" ukilinganisha na misimu iliyopita hasa ukiangalia umakini na nguvu ambayo Lakers wanaihitaji ili kufikia japo hatua ya mtoano. 

Ikumbukwe kuwa wakati Lebron akiwa kwenye kikosi cha LA LAKERS msimu huu walishinda mechi 22 na kupoteza 17. Lakini katika hizi wiki 5 ambazo alikosekana kwa sababu za kuwa majeruhi, Lakers wameshinda mechi 6 tu na kupoteza 12. 

Loading...

No comments: