LUIS SUAREZ APELEKA MSIBA MZITO BERNABEU WAKATI BARCA IKIWEKA HISTORIA KATIKA COPA DEL REY. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

LUIS SUAREZ APELEKA MSIBA MZITO BERNABEU WAKATI BARCA IKIWEKA HISTORIA KATIKA COPA DEL REY.

Fc Barcelona

Mshambuliaji wa klabu ya Fc Barcelona LUIS SUAREZ, jana usiku alikuwa chachu kubwa katika ushindi wa 3-0 walioupata dhidi ya Real Madrid katika mechi ya marudiano ya nusu fainali ya kombe la mfalme (Copa Del Rey) uliofanyika katika uwanja wa Santiago Bernabeu. 

Suarez ambaye alikuwa katika fomu mbaya sana msimu huu na katika mechi za hivi karibuni, alifunga magoli mawili katika mechi hiyo na kuwasambaratisha kabisa Los Blancos nyumbani kwao. Suarez alifunga magoli yake dakika ya 50 na 73 huku beki wa Real madrid, Verane akijifunga mnamo dakika ya 69. 

Winga wa Real Madrid Gareth Bale (kulia) akijaribu kumtoka beki wa kulia wa Fc Barcelona Nelson Semedo hapo jana.
Kwa matokeo hayo, Real madrid wametolewa rasmi na Fc Barcelona anatinga fainali hizo kwa mara ya 6 mfululizo na kuweka rekodi mpya hiyo ambayo hakuna timu iliyowahi kuingia fainali ya kombe hilo mara 6 mfululizo. 

FC BARCELONA wanamsubiri mshindi wa mechi kati ya Valencia na Real Betis inayochezwa leo huku timu hizo zikiwa zimeshafungana 2-2 kwenye mechi ya kwanza. 

Timu hizo zitakutana tena katika uwanja huo huo mnamo jumamosi hii tarehe 02/03/2019 katika mechi ya ligi kuu ya Hispania, LALIGA. 

Loading...

No comments: