Maadhimisho miaka 42 ya CCM Mkoani Morogoro - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 4, 2019

Maadhimisho miaka 42 ya CCM Mkoani Morogoro

CHAMA Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro , kimeadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama hicho kwa kufanya Shughuli mbalimbali  ikiwa ni   pamoja na Ujenzi wa kituo cha afya cha Mikumi, kuchangia vifaa vya ujenzi,
Kufanya usafi katika hospital ya wilaya ya kilosa na  kukabidhi vifaa vya wakinamama .

Katika Maadhimisho hayo  Mwenyekiti wa CCM mkoa Morogoro, Innocent Kalogeriz ameongoza na wana CCM kuwatembelea na kuzungumza na viongozi wa mashina, wazee na wanachama wagonjwa na kuwapatia vifaa mbali mbali.

Aidha Mwenyekiti aliongoza zoezi la uchangiaji damu na kisha kuzungumza na wanaccm  na viongozi kutoka wilaya  zote za mkoa wa Morogoro walioshiriki maadhimisho hayo.


Kupitia sherehe za miaka 42 ya CCM Mwenyekiti huyo ametangaza na kuzindua rasmi kampeni inayojulikana 
Operasheni Morogoro ya Kijani inawezekana ambayo imebeba kauli mbiu ya kuwa pamoja tusikubali kugawanyika 2019/2020.

Anasema Kampeni hiyo  itakayodumu hadi Octoba 2020 na kuhakikisha wanaccm wanashikamana ipasavyo

Katika maadhkmisho hayo pia  amepokea wanachama wapya 1, 000 kutoka vyama mbalimbali ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ACT  Wazalendo na Chama cha wananchi CUF pamoja na  kukabidhi vitendea kazi kwa mabalozi .

Anasema maadhimisho hayo yataendelea katika wilaya mbali mbali hadi februari 28,2019 katika madhimisho hayo yalihudhuriwa na wajumbe wa  kamati ya siasa ya Mkoa,  wilaya, mkuu wa mkoa wa Morogoro,  wakuu wa wilaya, wasanii  na viongozi mbali mbali wa chama na wadau wa maendeleo, yalipambwa na vikundi mbali mbali vya sanaa kutoka mkoa wa Morogoro na kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) kimkoa yamefanyika wilayani Kilosa Jimbo la Mikumi. 

Loading...

No comments: