Makamba anaamini Simba itetea ubingwa, atoa ushauri kwa viongozi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 22, 2019

Makamba anaamini Simba itetea ubingwa, atoa ushauri kwa viongozi


MAKAMBA, SIMBA ,YANGA,
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba ambaye pia ni mwanachama wa Simba itatetea ubingwa wake msimu huu lakini pia amewashauri baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wanaokosa weledi katika kutimiza majukumu yao.
“Simba itatetea ubingwa wake, ishara kubwa ilikuwa juzi maana ile mechi ilikuwa mechi ya pointi 6 sio 3 sisi tulishinda ambaye hatutaki ashinde kapoteza kwenye mechi hiyohiyo moja tulipata matokeo mawili, mshindani wetu kapoteza sisi tukapata pointi 3 kwa hiyo kikubwa tusibweteke unajua wachezaji wanaweza kujiona wamecheza CAF Champions League halafu ligi wakaichukulia kawaida.”
“Ili tupate uzoefu kwenye Champions League lazima tushinde ligi ili mwakani tushiriki tena Champions League, tuko vizuri.”


SIMBA VS AZAM
“Kama mwarabu kapigwa hapa Azam nani? Tumepiga Yanga usizungumze habari za Azam ambao zuji tu wamepigwa na Prisons.”


USHAURI KWA VIONGOZI WA SIMBA

“Mimi ni muumini wa mageuzi, lakini mageuzi yanaenda sambamba na utamaduni (structure & culture) muundo umebadilika lakini utamaduni wa uendeshaji mpira inabidi nao ubadilike, ujanjaujanja na utapeli, maneno yasiyo na maana na vitu kama hivyo inabidi tubadilishe.”
“Ukibadilisha tu muundo bila kubadili utamaduni hakuna chochote kitakachotokea. Nidhamu ya wachezaji, viongozi kutoingilia masuala ya ufundi na pia unapowasiliana na umma unatumia lugha gani na weledi kwenye klabu.”
“Hivi vitu (structure & culture) lazima viende pamoja, structure imefanikiwa kwa sababu kuna muundo mpya, katiba mpya, hisa na vingine kama bado mambo yaleyale ya ubabaishaji ambayo ndio yanatawala uendeshaji wa vilabu hapa Tanzania uwekezaji na haya mabadiliko yatakuwa hayana maana yoyote.”
“Kwa hiyo nawasihi viongozi wangu, tumebadilisha muundo tubadilishe na utamaduni.”

Loading...

No comments: