Makamu Wa Rais, Samia Suluhu Hassan Aongoza Mazishi Ya Mtoto Wa Waziri Kigwangalla - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 23, 2019

Makamu Wa Rais, Samia Suluhu Hassan Aongoza Mazishi Ya Mtoto Wa Waziri Kigwangalla


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan  ameongoza  shughuli za  mazishi  ya  Zulqarinain mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla  yaliyofanyika leo Ijumaa Februari 22, 2019 saa kumi jioni katika kijiji cha Puge,  Nzega vijijini jimboni kwa Waziri Kigwangalla.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na   viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya Mawaziri, Manaibu Waziri Wabunge pamoja  na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Marehemu Zul alifikwa na mauti  jana majira ya saa nne asubuhi   JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE katika hospitali ya taifa ya Muhimbili  alikokuwa   amelazwa   akiwa anasumbuliwa na tatizo la moyo.

#R.I.P Zul.

Inna lillahi wainna illaihi rajiuun

 

Loading...

No comments: