MAN CITY WAIRARUA CHELSEA, AGUERO AVUNJA REKODI KWA KUPIGA HATTRICK - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 10, 2019

MAN CITY WAIRARUA CHELSEA, AGUERO AVUNJA REKODI KWA KUPIGA HATTRICK


Mechi iliyomalizika muda si mrefu katika ligi kuu ya nchini Uingereza maarufu kama EPL ilikuwa ni kati ya Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola dhidi ya Chelsea ya kwake kocha Maurizio Sarri. Mchezo huo umemalizika huku matokeo yakiwa ni ushindi kwa Manchester City wa 6-0 na ya aibu kwa wababe wa jiji la London, Chelsea. 

 Man city walianza kwa kasi sana mchezo huo huku wakitawala vyema eneo la kiungo katikati mwa uwanja na hata haikuchukua muda mrefu kwa Raheem Sterling kufunga bao la kuongoza mnamo dakika ya 4 tu ya mchezo kwa shuti kali baada ya kukutana na mpira ulokuwa unazagaa kwenye lango la chelsea. 

Muuaji wa Chelsea leo alikuwa ni Mshambuliaji Muargentina Sergio Kun Aguero ambaye aliipatia Man City goli la pili na la tatu ndani ya dakika 7 tu (dk ya 13 na 19) magoli ambayo sio ya ubishi na ni magoli ambayo yamedhihirisha ubora wake. 

Wakati Sarri na wachezaji wake wakijiuliza imekuwaje tumeruhusu goli hizi tatu haraka namna hii, kiungo wa Man City Ikay Gundogan akaipatia Man City goli la nne kwa mkwaju mkali nje ya box na kufanya mpaka mapumziko iwe ni 4-0. 

Kun Aguero alifunga goli lake la tatu katika mchezo huo mnamo dakika ya 56 na kukamilisha HATTRICK kwa mkwaju wa penati. Hattrick hiyo inakuwa ni ya 11 kwake katika ligi kuu ya nchini Uingereza na amevunja rekodi ya gwiji wa Newcastle, Allan Shearer ambaye naye alikuwa na Hattrick 11 na hakuna mchezaji aliyewahi kuzifikia kabla. 

Aliyetupia msumari wa mwisho alikuwa ni Raheem Sterling katika dakika ya 80 na kufuta ndoto za COMEBACK kwa Chelsea pamoja na timu zilizokuwa zikitaka Chelsea washinde (Liverpool hasa). 

Ushindi huo unawafanya Manchester City kurudi kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa sawa point na Liverpool ambao hawajacheza mchezo mmoja bado. 

SWALI: Je nani atachukua Ubingwa msimu huu? 

Loading...

No comments: