MAN UNITED WANAANDAA DAU KUBWA KWA AJILI YA KOULIBALLY - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 17, 2019

MAN UNITED WANAANDAA DAU KUBWA KWA AJILI YA KOULIBALLY

Koulibaly to Man United

Imeripotiwa kuwa klabu ya Manchester United imeandaa dau la takribani pauni milioni 90 (Euro 102 milioni) kwa ajili ya kupata saini ya moja ya mabeki bora wa kati duniani kwa sasa anayechezea klabu ya Napoli Kalidou Koulibally. 

Lakini Msenegali huyo ameonyesha uzalendo kwa klabu yake ya sasa ya Napoli siku ya ijumaa aliposema "Nashangazwa na najisikia vizuri kujua hayo, lakini kwa sasa nimewekeza nguvu zangu kwa Napoli kuonyesha uwezo wangu uwanjani. Vipo vingi vya kunipa hamasa hapa Napoli, tunataka kuthibitisha kuwa tupo level ya juu na ninataka kuendelea kuboreka zaidi nikiwa hapa."

Koulibally aliyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha RAI SPORT siku ya ijumaa.
Loading...

No comments: