MAN UNITED YA OLE GUNNAR YAWEKA HISTORIA MPYA BAADA YA USHINDI DHIDI YA CRYSTAL PALACE HAPO JANA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

MAN UNITED YA OLE GUNNAR YAWEKA HISTORIA MPYA BAADA YA USHINDI DHIDI YA CRYSTAL PALACE HAPO JANA


Klabu ya Manchester United chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer jana iliweka rekodi mpya kabisa katika historia ya klabu hiyo baada ya kuishinda Crystal Palace 3-1 ugenini hapo jana. Magoli mawili ya mshambuliaji Romelo Lukaku na beki Ashley Young yalitosha kuihakikishia ushindi United ambayo ipo katika fomu na ari mpya kabisa. 

Rekodi mpya iliyowekwa jana ni ya kushinda mechi mfululizo za ugenini katika mashindano yote. Hakuna kocha wa United yeyote kabla aliyewahi kufanya hivyo. 

Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer akimpongeza kiungo Paul Pogba mara baada ya moja ya mechi zao.
United ambayo inaandamwa na majeruhi, bado imeendelea kufanya vyema na kuonyesha ukakamavu na ushupavu wa hali ya juu ambao ulikuwahauonekani chini ya kocha aliyepita JOSE MOURINHO. 

Loading...

No comments: