Man Utd wataja hasara waliyoipata kwa kumtimua Mourinho - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 15, 2019

Man Utd wataja hasara waliyoipata kwa kumtimua Mourinho


Klabu ya Manchester United imetaja kiasi cha gharama walizozikwaa baada ya kufanya maamuzi magumu Desemba mwaka jana ya kumtimua aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Jose Mourinho.

Klabu hiyo imeeleza kuwa hatua ya kumtimua Mourinho pamoja na benchi lake la ufundi lililokuwa na Silvino Louro, Carlos Lalin, Stefano Rapetti, Ricardo Formosinho na Giovanni Cerra kuliwagharimu kiasi cha £19.6 milioni (sawa na $25.1 milioni).

Uamuzi huo mgumu wa ulichukuliwa kufuatia mfululizo wa vipigo kwa timu hiyo pamoja na kuvurugika kwa umoja wa timu na uhusiano kati ya wachezaji muhimu na kocha huyo.

Nafasi ya Mourinho ilichukuliwa na Ole Gunnar Solskjaer aliyewahi kuwa mchezaji mahiri wa klabu hiyo, na ndani ya muda mfupi alionesha mabadiliko chanya na kufufua matumaini ya Manchester United hasa kwenye Ligu Kuu ya Uingereza. Tayari ameshajipatia ushindi katika michezo 10 kati ya 12 akiisogeza timu hiyo katika nafasi ya nne.

 [McKenna], Michael [Carrick] na Emilio [Alvarez], umeleta matokeo chanya kwenye timu yetu,” 
Ingawa waliingia gharama kubwa kufanya mabadilko ya benchi la ufundi, Manchester United iliingiza jumla ya $399.9 milioni katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2018.

No comments: