Manara na Mo Dewji Wakutanishwa na TFF


Manara na Mo Dewji Wakutanishwa na TFF
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limeunda Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde ikiwa na wajumbe 14 wakiwemo Jerry Muro pamoja na Haji Manara na muwezeshaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’.Kamati hiyo ambayo itaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ndiye mwenyekiti huku Mhandisi Hersi Said akiwa katibu.Kamati hiyo pia inaundwa na wajumbe wengine kama Mohammed Dewji ‘Mo’, Farouk Barhoza, Salim Abdallah,Mohamed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin Kleb, Teddy Mapunda, Philemon Ntahilaja, Farid Nahid na Faraji Asas.Kamati hiyo ya Saidia Taifa Stars ishinde imeundwa maalum kwa mechi dhidi ya Uganda mwezi ujao kuwania kufuzu Afcon.

Post a Comment

0 Comments