Marekani washambuliwa mkutano barani Ulaya - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 17, 2019

Marekani washambuliwa mkutano barani Ulaya


Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas ametoa wito wa kutafuta suluhisho kunakohusisha pande tofauti tofauti na kumshutumu Rais wa Marekani Donald Trump kwa kujichukulia maamuzi bila ya kushirikisha wengine.

Akizungumza jana jioni katika mkutano huo wa Munich, Maas aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kuongezeka kwa nguvu za China kunahitaji nchi za Ulaya na Marekani kufanya kazi kwa pamoja, akigusia pia hatua ya Trump ya kuongeza bei ya bidhaa za chuma kama jambo linalotishia nafasi za ajira Ulaya.

Waziri huyo ya mambo ya kigeni wa Ujerumani pia ameishutumu Marekani kwa kujiondoa kutoka mkataba wa kinyuklia uliofikiwa kati ya Iran na nchi zenye nguvu zaidi duniani akisema Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zinajaribu kuyadumisha makubaliano hayo kwani yakisambaratika, basi kanda ya Mashariki ya Kati huenda ikatumbukia katika mizozo zaidi.
Loading...

No comments: