MASHABIKI WA YANGA WAITWA TAIFA KUIPA SAPOTI SIMBA KIMATAIFA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 12, 2019

MASHABIKI WA YANGA WAITWA TAIFA KUIPA SAPOTI SIMBA KIMATAIFA


MBUNGE wa Jimbo la Iramba, na Raisi wa timu ya Singida United, Dr Mwigulu Nchemba, amewataka wale wa Yanga, Singida, Azam na timu zote kiujumla wenye tabia ya kuwashabikia wapinzani kuacha kufanya hivyo hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

Simba leo itakuwa uwanja wa Taifa ikicheza mchezo wa marudiano hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Nchemba amesema kuwa kwenye mashindano yote ya kimataifa huwa anaweka kando ushabiki na kutanguliza uzalendo mbele kwa manufaa ya Taifa.

" Simba ikifanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa itapata fursa ya kufungua milango kwa mafanikio, nchi yetu itaongezewa nafasi kama itafanikiwa kufika nusu fainaili itaongeza nafasi nne kama ambavyo Zesco ilifanya.

"Sasa kama ikifanya vizuri kwenye mashindano haya na kutinga hatua ya nusu fainali nafasi nne hawatashiriki wao wenyewe bali Yanga watakwenda, Azam FC watakwenda, Singida United watakwenda na timu nyngine, hivyo tunapaswa tuipe sapoti mashabiki wote," amesema.
Loading...

No comments: