Matibabu ya Ruge Mutahaba kwa siku Tsh Mil. 5 hadi 6, familia yaomba msaada - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 20, 2019

Matibabu ya Ruge Mutahaba kwa siku Tsh Mil. 5 hadi 6, familia yaomba msaada


Familia ya Ruge Mutahaba imeomba msaada wa fedha kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya Mkurugenzi huyo wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group.Akiongea kwa niaba ya familia, kaka yake na Ruge Mutahaba, Mbaki Mutahaba amesema kuwa kwa sasa Ruge anapatiwa matibabu Afrika Kusini ambako kwa siku gharama ni kuanzia Tsh milioni 5 hadi 6.
Alianza kuumwa mwaka 2018, alilazwa katika Hospitali ya Kairuki  kisha akapelekwa India, sapoti ni kubwa tunashukuru na hata Rais (John Magufuli)  ametoa mchango na anaendelea,“amesema Mbaki katika mahojiano yake na kituo cha Televisheni cha Clouds na kueleza kinachomsumbua.
Ana figo ambayo haipo sawasawa ilikuwa lazima wambadilishe. Madaktari wa hospitali ya Kairuki na Muhimbili wakashauri apelekwe Afrika Kusini maana ni karibu zaidi lakini gharama ni kubwa.“amesema Mbaki.
Gharama za matibabu kwa kule ni kubwa na kwa siku inaweza kufika million 5 mpaka 6, kuna number ambayo imeandikishwa kwa jina la mdogo wetu, Kemilembe Mutahaba 0752 222 210 hiyo ndiyo number ambayo watu wanaweza kutuma sms za pole, faraja na hata wengine ambao wangetamani kutuma chochote”. Mbaki Mutahaba
Loading...

No comments: