MATIC: "MAN UNITED HAINA CHA KUPOTEZA, TUNAPELEKA MAPAMBANO JIJINI PARIS" - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 13, 2019

MATIC: "MAN UNITED HAINA CHA KUPOTEZA, TUNAPELEKA MAPAMBANO JIJINI PARIS"Kiungo mkabaji wa klabu ya Manchester United, Mserbia, Nemanja Matic anaamini timu yake haina cha kupoteza kufuatia kipigo cha mabao 2-0 nyumbani dhidi ya klabu ya Paris Saint-German hapo jana na anaamini kuwa watajipanga vyema kwenda kupindua matokeo katika mchezo wa marudiano kule jijini Paris, Ufaransa. 

Mashetani hao wekundu wamekuwa katika form nzuri ya kutopoteza mechi 11 chini ya kocha wao mpya Ole Guna Solskjaer mpaka hapo jana walipokutana na kichapo chao cha kwanza. 

Akihojiwa baada ya mechi, Matic alisema "PSG walikuwa na nafasi nyingi na sisi tulikuwa pabaya, lakini tunapaswa kuwaheshimu, wana wachezaji wakubwa, ni timu kubwa."

"Tutakwenda Paris kujaribu vitu kadhaa. Hatuna cha kupoteza kwahiyo tutakwenda pale kucheza mpira mzuri na kujaribu kushinda."


Loading...

No comments: