Mbosso aweka wazi bifu lake na Aslay “alini-unfollow na mimi nikam-unfollow kubalance shobo” - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 24, 2019

Mbosso aweka wazi bifu lake na Aslay “alini-unfollow na mimi nikam-unfollow kubalance shobo”


Msanii wa muziki kutoka WCB, Mbosso ameweka wazi kwamba kwa sasa hayupo sawa na muimbaji mwenzake, Aslay ambaye awali alikuwa anafanya naye kazi katika bendi ya Yamoto Band.


Mbosso wakati anaongea na Azam, alisema awali alikuwa anamsupport Aslay katika kazi zake ambazo amekuwa akizitoa lakini yeye amedai alikuwa hasapotiwi na muimbaji huyo.

“Baada ya kumsupport Aslay kwa muda mrefu watu wakawa wananimbia mbona wewe unam-support halafu yeye haku-support? umem-follow mwenzako ameku-unfollow. Jifunze kubalance shobo, nikasema kumbe na mimi naonekana namshobokea ngoja na mimi nim-unfollow. Kwa hiyo sasa hivi kila mtu hana urafiki na mwenzake,” alisema Mbosso.
Loading...

No comments: