Mbunge afungwa kisa Twitter

Mbunge na aliyekua waziri wa zamani wa michezo Ivory Coast, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kusambaza taarifa za uongo kupitia ukarasa wake wa Twitter. 
Alain Lobognan aliandika katika ukurasa wake wa Twitter tarehe 9 Januari kuwa mkuu wa upelelezi ametoa tamko la kukamatwa kwa mbunge mwenzake, taarifa hiyo ilizua gumzo na fujo kwa miongoni wa wafuasi wa mbunge huyo. 
Lakini mkuu wa upelelezi alikanusha kutoa tamko hilo kama alivyoandika Lobognan katika ukurasa wake wa Twitter. 


Mbunge huyo ambaye yupo katika mgomo wa kula siku ya kumi sasa anasema kuwa kesi yake imeingiliwa kisiasa. 
Mwanasheria wake bi Affoussiata Bamba Lamine, amesema kuwa wana mpango wa kukata rufaa. 
Ameongeza pia kuwa kesi ya mteja wake imeingiliwa kisiasa, na kusema kuwa analengwa kwasababu ya ukaribu wake waziri mkuu wa zamani na alikua pia kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro. 
Kwasasa ni spika wa bunge, mwezi uliopita kiongozi huyo alitangaza kuachia madaraka kama spika. 
Wachambuzi wanasema kuwa huenda ameanza kujiandaa na kugombea urais mwaka 2020.

Post a Comment

0 Comments