Mbwana Samatta moto wake haushikiki Ubelgiji kwa sasa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 9, 2019

Mbwana Samatta moto wake haushikiki Ubelgiji kwa sasa


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayekipiga katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji ameenedelea kuwa moto katika safu ya ushambuliaji ya KRC Genk, kufuatia kuiongoza kujipatia point tatu muhimu katika mchezo dhidi ya Standard de Liege wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.


Mchezo huo wa 25 uliyochezwa katika uwanja wa Luminus ambao ndio uwanja wa nyumbani wa KRC Genk, umemalizika kwa KRC Genk kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli ambayo yote mawili yamefungwa na Mbwana Samatta dakika ya 67 na 87 na kuvuna point 3.

Licha ya ushindi  huo Mbwana Samatta magoli hayo yanamfanya kuendelea kuongoza katika list ya wafungaji wa magoli katika Ligi Kuu Ubelgiji, kwa kufikisha jumla ya magoli 19 akifuatiwa na Hamdi Harbaoui wa Zulte-Waregem mwenye magoli 14, Samatta sasa anaongoza kwa tofauti ya magoli 5 na anaweza kutwa kiatu cha dhahabu kutokana na mwenendo wake.
Loading...

No comments: