MCHEZAJI HUYU SIMBA AKIKUFUNGA TU, LAZIMA UPIGWE NYINGI TU, CHEKI TIMU ALIZOZITUNGUA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 25, 2019

MCHEZAJI HUYU SIMBA AKIKUFUNGA TU, LAZIMA UPIGWE NYINGI TU, CHEKI TIMU ALIZOZITUNGUA


NAHODHA wa Simba, John Bocco ameweka rekodi ya aina yake katika michezo aliyopata nafasi ya kuifungia timu yake kwani mechi zote alizofunga Simba ilishinda mabao matatu.

Bocco ambaye msimu uliopita alitupia mabao 14 na msimu huu aliliambia SpotiXtra kuwa atafunga mabao mengi zaidi ya hayo alianza kwa kusuasua kutokana na kusumbuliwa na majeruhi na alifungulia bao lake la kwanza kwenye mchezo wake dhidi ya Mwadui.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex Bocco alifunga mabao mawili na bao la tatu likafungwa na Meddie Kagere na kufanya Simba ishinde mabao 3-1.

Pia katika mchezo wake dhidi ya Singida United, Bocco aliifungia timu yake na ilishinda mabao 3-0, pia kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Mwadui Bocco alifunga bao moja na kuiongoza Simba kushinda mabao 3-0.

Hakuishia hapo mchezo wake dhidi ya African Lyon alitupia mabao mawili na mchezo ulikamilika kwa mabao 3-0, juzi aliendeleza rekodi hiyo baada ya kuwatungua mabosi wake wa zamani Azam FC Simba ilishinda mabao 3-1, rekodi hii haijawekwa na nahodha yoyote bongo kwa sasa.

Bocco mpaka sasa ana mabao saba huku timu yake ikiwa imefunga mabao 38 ikiwa nafasi ya tatu na pointi 45, Azam wapo nafasi ya pili na pointi 50, wakiachwa nyuma na wapinzani wao Yanga ambao ni vinara wenye pointi 61.
Loading...

No comments: