Mchezaji wa Tanzania Himid Mao azidi kung'ara Misri - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 27, 2019

Mchezaji wa Tanzania Himid Mao azidi kung'ara MisriKiungo mkabaji na Nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Himid Mao Nkami anaendeleza harakati zake za kucheza soka la kulipwa nchini Misri akiitumikia Klabu ya Petrojet inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo, Himid jana alikuwa Uwanjani kucheza dhidi ya Daklyeh.

Himid Mao ameisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dakiyeh na kuondoka na alama tatu katika Uwanja wa ugenini hivyo kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri zaidi katika Ligi Kuu nchini Misri inayoshirikisha jumla ya timu 18, alifunga bao moja katika ushindi huo na kufikisha jumla ya mabao matatu.

Hadi sasa Himidi Mao ana mabao matatu na pasi tatu za usaidizi wa mbao akiwa ameisadia timu yake kupanda katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Misri hadi kuwa nafasi ya 12 kati ya timu 18 zinazoshiriki Ligi hiyo wakiwa na alama 25 sawa na Samouah waliopo nafasi ya 13, Petrojet wako na tofauti ya alama nne kutoka sehemu ya hatari ya kushuka daraja hivyo wanaendeleza kupigana kujiweka nafasi nzuri.
Loading...

No comments: