Meneja wa WCB Atoa Tamko Kuhusu Harmonize - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 21, 2019

Meneja wa WCB Atoa Tamko Kuhusu Harmonize


Meneja wa WCB Atoa Tamko Kuhusu Harmonize
Meneja kutoka WCB, Sallam SK leo amefunguka kuwa EP ya Harmonize, AfroBongo haitatoka tena wiki hii kama ilivyokuwa imepangwa awali bali itatoka wiki ijayo.

Pia Meneja Sallam SK ameweka wazi sababu zilizopelekea kupelekwa mbele kwa tarehe ya kuachiwa kwa project hiyo kwa kueleza kilichochangia zaidi ni sababu za kibiashara.

“Kama uongozi lazima tumuandalie misingi ya kibiashara ili anufaike na kazi zake pia, na vilevile tusiwe na matabaka ya kuwajali mashabiki wa sehemu moja pale kazi zinapotoka, inatakiwa kama uongozi kuhakikisha kazi ya msanii inapatikana sehemu zote kukidhi hamu za mashabiki wote," ameeleza.

"Kingine unapofanya kazi na wasanii waliopo lebo kubwa inahitajika lebo zao waweze kutia saini mikataba ya mirabaha ili nyimbo ziweze kuwepo kwenye mitandao yote ya mauzo ili isilete matatizo kwenye lebo zao," amesema Sallam SK.

Sallam SK amehitimisha kwa kueleza kuwa  ukubwa wa EP ya Harmonize ilihitaji kupitia yote hayo ili iwe tayari kufika kwa mashabiki, huku awashukuru Basata kwa kutoa ushirikiano mzuri kuzikagua nyimbo kwa muda muafaka na hakutokua na tatizo la wimbo unatoka halafu unafungiwa.

Loading...

No comments: