MKASA MZIMA WA MWAMUZI ODEN MBAGA KUFUNGIWA MAISHA NA FIFA KUTOJIHUSISHA NA SOKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

MKASA MZIMA WA MWAMUZI ODEN MBAGA KUFUNGIWA MAISHA NA FIFA KUTOJIHUSISHA NA SOKA


Zurich, Uswisi. Shirikisho la Soka Duniani Fifa limemfungia maisha mwamuzi wa Tanzania, Oden Charles Mbaga kwa kosa la kuchukua rushwa. 

Fifa imesema Mbaga pia atatozwa faini ya dola 200,000. Haijulikani ni jinsi gani Fifa inaweza kutoza faini kwa makossa ya utovu wa nidhamu.

Bila ya kuweka wazi kuhusu rushwa hiyo, Fifa ilisema Mbaga alitenda kosa hilo 2009, uchunguzi wa suala lake ulianza kufanywa Julai mwaka jana. 

Mbaga ameripotiwa kuhusika na shtuma za upangaji wa matoke Wilson Perumal, Singapore, ambao walihusika na kutoa hongo kwa waamuzi waliochezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa na kuhusika kwa michezo ya kubahatisha. 

Mbaga amekuwa katika orodha ya waamuzi wa Fifa wanaochezesha mechi za timu za taifa.


MKASA MZIMA UPOJE KWANI?
Katika mahojiano aliyofanya na gazeti la Mwananchi mwaka 2016, mwamuzi Mbaga alisimulia mkasa wote.

Wakufunzi wa waamuzi, Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini na Felix Tangawarima wa Zimbabwe wametajwa kama kiini cha kuzimwa ndoto za waamuzi Oden Mbaga, Hamis Chang’walu na Jesse Erasmo. 

Katika mwendelezo wa mahojiano yake na gazeti hili, mwamuzi Mbaga alisema kuwa wakufunzi hao ndiyo waliozusha taarifa kuwa yeye na wenzake wanahusika na upangaji wa matokeo kwenye mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa. 

Waamuzi hao watatu walisimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kile kilichotajwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za upangaji wa matokeo zilizokuwa zikiwakabili. 

Chanzo cha haya yote ni Carlos Henrique na Felix Tangawalima, wakufunzi wa waamuzi wa soka Kanda ya Kusini mwa Afrika. 

Huyu Carlos ndiye chanzo kikubwa cha waamuzi wa Tanzania kupotea akiwa na mwingine anaitwa Felix Tangawalima kutoka Zimbabwe,” alisema Mbaga. 

Mbaga alisema Julai 10, 2014 wakufunzi hao wakati wa kozi ya waamuzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam walimuita ofisini na kuanza kumuhoji tuhuma mbalimbali, ikiwamo upangaji wa matokeo. 

Wakati wa kipindi cha pili cha mazoezi, akaja Felix akasema, sasa nina jina lako lipo hapa. Wewe ni mmoja wa waamuzi vijana wa Afrika, jina lako nimelipendekeza ukachezeshe fainali za vijana ya Kombe la Dunia. 

“Tulikuwa tunaelewana, lakini kuna jambo nataka unisaidie, twende kwenye ofisi za TFF, kufika huko nikamkuta Carlos ambaye akiwa na kompyuta yake wakaanza kuniuliza ilikuwaje ukaenda Afrika Kusini, nikawajibu na kuwapa mtiririko mzima ulivyokwenda,” alieleza Mbaga. 

Mwamuzi huyo alisema kwa undani jinsi alivyopata mwaliko kwenda Afrika Kusini kuchezesha mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Denmark. 

Hata hivyo, akiwa huko, alishindwa kuchezesha mchezo huo kutokana na kuugua tumbo ghafla, ingawa wenzake wawili, Erasmo na Chang’walu walichezesha wakishirikiana na mwamuzi kutoka Afrika Kusini.

Mbaga alisema kuwa baada ya kuwajibu, wakufunzi hao walimhoji anafahamiana vipi na mtu anayeitwa Wilson. 

“Akaniuliza kuna bwana mmoja anaitwa Wilson unamjua? Hujawahi kukutana naye? Nikasema huyu mtu sijawahi kukutana naye, ila nina rafiki ni raia wa Singapore niliyekutana naye Uganda wakati nachezesha mechi za mpira wa kikapu.”

Alisema kuwa raia huyu wa Singapore alivutiwa na uchezeshaji wake na kumpa mawasiliano yake akidai ana mpango wa kuja Tanzania kusaka vipaji vya michezo kwa vijanai. 

Mbaga alisema baadaye mwaka huo alikutana na raia huyo wa Singapore wakati alipokuwa anachezesha mashindano ya Chalenji yaliyofanyika Kenya. 

“Alivyoniona, akaniuliza kumbe hata mpira wa miguu unachezesha? Nikamwambia ndiyo. Akaniambia, basi wewe utatusaidia kwenye kampuni ya baba. Akaniambia naomba simu yako baadaye tuzungumze. 

Baadaye akaniambia: “ Kampuni ya baba inashughulika na mambo ya michezo. Duniani kote inakubalika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Unaonaje nawe ukiwa mmoja wa waamuzi ukanufaika na programu hiyo kwa sababu wewe bado kijana na hiyo michezo itakusaidia,” alisema Mbaga. 

Aliongeza kuwa baada ya kuwapa majibu hayo bado walimuuliza maswali mengine, ikiwamo jinsi alivyokwenda Afrika Kusini na kiasi cha fedha alichopata, mali anazomiliki na maisha yake kwa jumla. 

Bila kujua kinachoendelea, Mbaga alisema alikuwa anarekodiwa kisirisiri na Carlos ambaye baadaye alikwenda kumtuhumu kwa viongozi wa TFF kuwa anahusika na upangaji wa matokeo kwa kushirikiana na wacheza kamari. 

Kwa mujibu wa Mbaga, uongozi wa TFF chini ya Rais Leodegar Tenga, haukukubaliana na ushahidi waliopewa na Carlos na mwenzake kwa kuwa haukuwa na mashiko. 

Baada ya Tenga kuwakatalia, wale mabwana wakaondoka, kumbe walivyotoka hapa (Tanzania) walikwenda Zurich, Uswisi kufika kule wakapeleka ile sauti waliyokuwa wananirekodi wakampa mkuu wa waamuzi duniani, Fernando Tresaco. Akaisikiliza, akasema ni vitu vya kawaida. 

Fifa wakawapuuza, wakaona haina mashiko. Wale mabwana wakawa wamekata tamaa, hawawezi kunitoa kwenye jopo la Fifa kwa hiyo sasa wakawa wamebaki kuzungumza na meneja wa waamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Eddy Maillet ambaye ni rafiki yake Carlos kuwa yeye, Erasmo na Chang’walu wasiwe wanapangiwa mechi,” alisema mwamuzi huyo. 

Alifichua kuwa baada ya kuona wamekaa muda mrefu bila kupangiwa mechi za kimataifa, Chang’walu aliwasiliana na mkufunzi wa waamuzi kanda ya Afrika Mashariki, Charles Masembe wa Uganda kujua kwa nini imekuwa hivyo. Loading...

No comments: