MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI ATEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA SGR KUTOKA KITO CHA ILALA HADI KILOSA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI ATEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA SGR KUTOKA KITO CHA ILALA HADI KILOSA


 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) jijini Dar es salaam, kabla ya kuanza ziara ya kutembelea Mradi huo kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Kilosa mkoani Morogoro. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiangalia sehemu ya reli ya Kisasa SGR iliyokamilika wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Kilosa mkoani Morogoro. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwasilia katika kituo cha Soga kilichopo mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuona namna mataluma ya reli yanavyotegenezwa katika kituo hicho wakati alipofaya ziara ya kutembelea Mradi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Kilosa mkoani Morogoro. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (kushoto) akimuelezea jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, kuhusiana na Mradi wa Reli ya kisasa SGR, wakati alipofanya ziara ya kutembelea Mradi huo unaojegwa na Kampuni ya Yapi Merkezi. Picha na Jeshi la Polisi.
Loading...

No comments: