MZEE WENGER: KUONDOKA KWA RAMSEY NI PIGO KWA ARSENAL - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 18, 2019

MZEE WENGER: KUONDOKA KWA RAMSEY NI PIGO KWA ARSENAL


Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal mzee Arsene Wenger amefunguka na kusema kuwa kiungo Aaron Ramsey atakuwa ongezeko la thamani sana katika klabu ya Juventus na kuondoka kwake ni pigo kwa klabu ya Arsenal. 

Ramsey mwenye miaka 28 atajiunga na klabu ya Juventus kwa uhamisho wa bure mwisho wa msimu ambao ni majira ya joto baada ya kukamilisha kusaini mkataba wa awali na mabingwa hao wa ligi kuu ya nchini Italia (SERIE A). 

'Rambo' amecheza chini ya Mzee Wenger kama kocha wake kwa muda wa miaka 10 na wawili hao wamefurahia mafanikio kadhaa ikiwemo kutwaa kombe la FA mara 3 huku Ramsey akifunga magoli ya ushindi katika fainali 2 kati ya hizo 3. 

Akiongea katika Laureus Sport For Good Presentation, mzee Wenger alisema: "Itakuwa ni pigo kwa ARSENAL. Ni lazima niseme kuwa utakuwa ni uhamisho mzuri kwa Ramsey mwenyewe. 

Aaron Ramsey akiwa mazoezini enzi za kocha Arsene Wenger


"Ni mchezaji mashuhuri kwa kwenda mbele kushambulia. Ubora wake mkuu ni uwezo wake wa kuulinda mpira na kukimbia kutokea chini sana au katikati na kupandisha timu. 

"Ni ngumu kuwapata wachezaji kama yeye leo ambao wana uwezo wa kuwafanya viungo wa timu pinzani wasipate mpira. Atakuwa ni ongezeko zuri kwa Juventus hakika." Alimaliza Wenger.

Loading...

No comments: