Neymar asherehekea birthday yake kwa staili ya aina yake (+picha) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 5, 2019

Neymar asherehekea birthday yake kwa staili ya aina yake (+picha)

Nyota wa klabu ya Paris Saint Germain na timu ya taifa ya Brazil, Neymar amesherehekea siku yake ya kuzaliwa hapo jana jioni siku ya Jumatatu katika jiji la Paris huku akiwa na magongo mkononi hii ni kufuatia kupata majeraha uwanjani. Hii si mara ya kwanza kuwa katika hali hiyo ya kutumia magongo kila inapofika siku yake ya kuzaliwa.


Mchezaji huyo ghali zaidi duniani, Neymar hapo jana amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na baadhi ya nyota wenzake wa PSG baada ya kutimiza miaka 27.

Neymar celebrated his 27th birthday with a glittering party in Paris on Monday evening


DJ maarufu nchini Ufaransa, Christophe Le Friant a.k.a Bob Sinclar, muimbaji kutoka Brazil, Wesley Safadao na bingwa wa kuogelea kutoka Brazil, Gabriel Medina walikuwa ni miongoni mwa wageni 200 waliyoalikwa katika kunogesha usiku huo wa hapo jana kwenye birthday ya Neymar.

Dani Alves attended his Paris Saint-Germain team-mates' birthday on Monday evening

Dani Alves akiwa amewasili kwenye sherehe za staa huyo wa 

Nguo za rangi nyekundi ndio zilipamba usiku wa birthday wa nyota huyo Mbrazil.

Marco Verratti and Gianluigi Buffon also turned up and kept up with the 'red night' theme

Marco Verratti na Gianluigi Buffon pia walihudhuria sherehe hizo za usiku wa nguo nyekundu

Miongoni mwa watu wengine waliyohudhuria ni pamoja na nahodha, Thiago Silva pamoja na mlindalango, Alphonse Areola.

Angel Di Maria turned up his team-mate's 27th birthday party with his wife Jorgelina Cardoso

Angel Di Maria turned akiwa naye amehudhuria akiwa na mke wake Jorgelina Cardoso

Neymar ambaye ametimiza miaka 27 siku ya Jumanne, ataikosa michezo miwili ya Paris Saint-Germain kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Manchester United kufuatia kupata majeraha kwenye kifundo chake cha mguu mwezi uliyopita.
Neymar amejikuta akiwa kwenye siku nzuri ya kuzaliwa ambayo ni Jumanne kufuatia kuzaliwa mwezi na tarehe sawa na nyota hawa wakubwa, Cristiano Ronaldo akitimiza miaka 34, Carlos Tevez miaka 35, na Gheorghe Hagi mwenye miaka 54 hawa wote wakiwa wamezaliwa Februari 5. 
Loading...

No comments: