Ni hatari kucheza mchezo wa wazi dhidi ya Waarabu - Haji Manara - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 3, 2019

Ni hatari kucheza mchezo wa wazi dhidi ya Waarabu - Haji Manara


Ni hatari kucheza mchezo wa wazi dhidi ya Waarabu - Haji Manara
Msemaji wa Simba SC, Haji Manara amefunguka kuhusu mchezo wa timu hiyo katika Ligi Mabigwa Afrika leo dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Haji amesema iwapo wachezaji watacheza kwa kujitoa zaidi wanaweza kuandika historia nyingine kwa waarabu.

"Ninachokiamini kocha wetu atakuja na mfumo sahihi wa kucheza kwa kuwaheshimu Ahly,
Yes ni hatari sana kucheza open game dhidi ya waarabu ukiwa ugenini," ameeleza.

Utakumbuka kuwa Simba SC itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi AS Vita ya DR Congo kwa kulala kwa goli 5-0. Hadi sasa Simba inashika nafasi ya tatu kwenye kundi lao ikiwa na pointi tatu sawa na AS Vita.
Loading...

No comments: