NI 'TEAM LEBRON' Vs 'TEAM GIANNIS' KATIKA NBA ALL STAR MWAKA HUU


Michezo ya NBA ALL STAR inarudi katika mji wa Charlotte kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991 huku watu wakisubiri kwa hamu mpambano kati ya 'Team Lebron' na 'Team Giannis'. 

Mwaka jana ulitambulishwa mfumo mpya wa kuandaa timu za kucheza mchezo huo wa ALL STAR ambapo huchaguliwa makapteni wawili ambao nao huchagua wenzao wawatakao kuunda vikosi viwili vitakavyomenyana siku ya mpambano. Hii ni tofauti na mfumo wa zamani ambao ulipambanisha wachezaji wanaotokea kanda ya magharibi 'TEAM WEST' na wale wanaotokea kanda ya mashariki 'TEAM EAST'. 

Mpaka sasa Team Lebron ina wachezaji wafuatao, 
KIKOSI KINACHOANZA: Lebron James mwenyewe, Kyrie Irving, Kevin Durant, James Harden, Kawhi Leonard, 
WA AKIBA: Anthony Davis, Klay Thompson, Damian Lillard, Ben Simons, Lamarcus Aldridge, Karl-Anthony Towns, Bradley Beal na Dwyane Wade.


Team Giannis ina wachezaji wafuatao,
KIKOSI KINACHOANZA: Giannis Antetokounmpo mwenyewe, Paul George, Joel Embiid, Kemba Walker, na Stephen Curry.
WA AKIBA: Khris Middleton, Nikola Jokic, Rusell Westbrook, Blake Griffin, D'Angelo Rusell, Nikola Vucevic, Kyle Lowry, Dirk Nowitzki.  


Mchezo huo utachezwa kesho kuanzia mida ya saa 10 usiku kwa masaa ya Afrika mashariki. 

Post a Comment

0 Comments