OLE GUNNAR SOLSKJAER: "FRED ATAPATA NAFASI YAKE KUNG'AA MAN UNITED"


Kocha wa muda wa klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa kiungo wake mbrazil FRED atapata muda wake wa kufanya mambo makubwa klabuni hapo lakini kwasasa anahitaji muda ili kuzoea mazingira na presha ya ligi kuu ya Uingereza. 

Fred ambaye ni mchezaji wa tano ghali zaidi katika kikosi cha Man United, alijiunga katika dirisha kubwa la usajili la kiangazi lakini bado hajaonyesha makali yake na hata mechi anazocheza zimekuwa ni chahe mno huku akianzishwa katika mechi saba tu katika ligi kuu ya Uingereza. 

Kiungo Fred akiugulia maumivu katika moja ya mechi za United

Katika hizo mechi saba alizoanza, ni moja tu ndio imetokea ikiwa chini ya kocha huyu mpya na ilikuwa wakati wa mechi dhidi ya Hurdesfield. Na kiujumla mbrazil huyo hajacheza hata dakika moja toka ushindi wa mechi ya United dhidi ya Reading katika kombe la FA mnamo januari 5.  

Post a Comment

0 Comments