PAUL DICKOV: HERERA NI SHUJAA ASIYEONGELEWA KAMA FERNANDINHO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 21, 2019

PAUL DICKOV: HERERA NI SHUJAA ASIYEONGELEWA KAMA FERNANDINHO

Ander Herera

Wakati akikaribia kusaini mkataba mpya wa miaka 3 wa kumbakiza OLD TRAFFORD, kiungo wa klabu ya Mnchester United Ander Herera ameonekana kama ni shujaa asiyeongelewa kwa watu wengi hasa Paul Dickov. 

Dickov anasema wakati mastaa wakubwa kama Paul Pogba na Anthony Martial wakichukua vichwa vya habari kila siku, Ander Herera ndio chacvhu kubwa ya mafaniko ya eneo la kiungo katika kikosi cha kocha wa mpito Ole Gunnar Solskjaer. 

Manchester United

Dickov alienda mbali zaidi kwa kumfananisha Ander Herera na kiungo mkabaji wa Manchester City, Fernandinho kwa namna ambavyo na yeye huwa haongelewi sana ila akikosekana kwenye mechi ndipo unaona umuhimu wake. 

Akihojiwa na kipindi cha THE DEBATE, Dickov alisema: "Ninadhani kuwa Herera ni sehemu muhimu mno ya kile Solskjaer amekuwa akijaribu kukifanya tangu amekuja hapa. Yeye ndio mtu muhimu pale na shujaa asiyeongelewa. Anafanya kazi kama anayofanya Fernandinho katika Manchester City. Amegeuka na kuwa kiongozi mkubwa sana."


Loading...

No comments: