PEP AISIFIA TEKNOLOJIA YA VAR BAADA YA USHINDI DHIDI YA SCHALKE 04 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 21, 2019

PEP AISIFIA TEKNOLOJIA YA VAR BAADA YA USHINDI DHIDI YA SCHALKE 04

Guardiola

Kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amewashangaza watu wengi kwa mtazamo chanya aliouonyesha dhidi ya teknolojia ya VAR ambayo hapo jana iliamua kupatikana kwa penati 2 dhidi ya timu yake. 


"Mimi ni shabiki mkubwa wa VAR. Ya kwanza ni penati na ya pili nayo ilikuwa penati pia." Alisema Guardiola baada Schalke kupata penati mbili dhidi ya City hapo jana usiku ambazo ziliwapa magoli 2 na kuwafanya waongoze kwa muda mrefu kabla ya Leroy Sane na Raheem Sterling hawajapindua matokeo.

SANE
Winga wa MANCHESTER CITY, Leroy Sane akipiga mpira wa adhabu uliosawazisha na kuwa 2-2 VS Schalke 04

Guardiola aliongeza kwa kusema kwamba VAR inahitaji muda zaidi na siku zinavyozidi kwenda mbele itaboreshwa na kuwa bora zaidi. 

Loading...

No comments: