PLUIJM ATAKIWA KUONDOKA AZAM - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 22, 2019

PLUIJM ATAKIWA KUONDOKA AZAM


Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara leo kati ya Simba dhidi ya Azam FC, baadhi ya mashabiki wa wekundu wa Msimbazi wameahidi kumfukuzisha Kocha Hans van der Pluijm.

Shabiki na mwanachama mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Ayoub Kawea, ameeleza kuwa mechi ya leo ndiyo itakuwa safari ya kwaheri kwa Pluijm.

Akizungumza kupitia Radio One, shabiki huyo anaamini kuwa Simba itapata matokeo na akieleza Azam hawana ubavu wa kuwazuia kwa chochote kile.

Aidha, ameongeza kuwa Simba inawaheshimu Azam ila kwa mchezo wa leo inabidi wawaasamehe tu kwakuwa wanahitaji alama tatu kuendelea kusaka mbio za ubingwa.

Simba na Azam zitakutana Uwanja wa Taifa saa 10 jioni leo ambapo mechi hiyo itakuwa LIVE kupitia Azam TV
Loading...

No comments: