POCHETTINO: ITACHUKUA MIAKA ZAIDI YA 10 KWA TOTTENHAM KUCHUKUA UBINGWA WA LIGI


Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amesema inaweza ikachukua miaka 5 hadi 10 kwa kikosi chake cha Spurs kuja kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza mara baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya timu ya Burnley. 

Mara tu baada ya timu yake kuchapwa mabao 2-1 na Burnley, Muargentina huyo alihitimisha kwa kusema kuwa changamoto na ushindani waliokuwa wanautoa umefika mwisho kwani wamepoteza nafasi ya kupunguza pointi 2 za utofauti kati yao na vigogo Manchester city pamoja na Liverpool ambao wanaongoza ligi. 

Poch alienda mbali zaidi kwa kujaji usawa wa kiakili wa wachezaji wake kwani wamekuwa wakipoteza michezo ambayo ingewapa nafasi ya kuongoza ligi au kushinda taji kwa misimu kadhaa sasa. 


Post a Comment

0 Comments