R Kelly afunguliwa mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingoni kwa watoto - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 25, 2019

R Kelly afunguliwa mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingoni kwa watoto
Msanii wa muziki nchini Marekani, Robert Sylvester Kelly a.k.a R Kelly amefunguliwa mashtaka 10 ya uanyanyasaji kingono watoto wadogo.

Mahakama ilichukua hatua hiyo baada ya ukanda wa video kuonesha tukio lililotokea 1998 na kuhusisha wasichana wanne.

R Kelly mwenye umri wa miaka 52 alijisalimisha kwa polisi mjini Chicago baada ya kibali cha kukamatwa kwake kutolewa.

Mahakama ya Chicago siku ya Ijuma ilitoa amri ya kukamatwa kwa mwanamuziki wa R&B R.Kelly kufuatia ushahidi mpya kuhusiana na madai aliwadhulumu kimapenzi watoto kati ya miaka 13-17.

Loading...

No comments: