Rais Magufuli amtembelea Charles Kitwanga Hospitali - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 3, 2019

Rais Magufuli amtembelea Charles Kitwanga Hospitali


Rais Magufuli amtembelea Charles Kitwanga Hospitali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemjulia Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Utakumbuka January 31 mwaka huu Spika wa Bunge  Job Ndugai aliagana na Mbunge huyo katika Uwanja wa Ndege wa Jijini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa  matibabu zaidi.

Charles Kitwanga aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika serikali hii ya awamu tano, May 2016 Rais alitengua uteuzi wake kiwa ni siku chache baada ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake ya mwaka 2016/17.

Loading...

No comments: