Rais Trump kukutana na rais Kim Jong-un kwa mara ya Pili - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 6, 2019

Rais Trump kukutana na rais Kim Jong-un kwa mara ya Pili

Rais Trump amethibitisha kwamba atakutana kwa mara ya pili na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Februari 27 na 28 nchini Vietnam.

 Viongozi hao walikutana kwa mara ya kwanza mwezi June mwaka 2018 nchini Singapore.

Katika hotuba kwa taifa iliyoambatana na kauli mbiu "Choosing Greatness", aliapa kwa mara nyingine kujenga ukuta mpakani.

Huku akihimiza umoja, kiongozi huyo wa Republican pia amesema jitihada za 'uchunguzi ulio na upendeleo' wa Democratic huenda ukaathiri ustawi wa Marekani.

Hotuba hiyo kuu ya rais Trump imejiri baada ya pengo la muda mrefu kuwahi kushuhudiwa katika historia, la kusitishwa ufadhili kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.
Loading...

No comments: