RAPA GODZILLA AFARIKI DUNIA GHAFLA USIKU WA KUAMKIA LEO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 13, 2019

RAPA GODZILLA AFARIKI DUNIA GHAFLA USIKU WA KUAMKIA LEO


Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Hip Hop GOLDEN JACOB MBUNDA maarufu kama GODZILLA amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwao Salasala Jijini Dar na mwili umehifadhiwa Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Zilla Atakumbukwa kwa vibao vyake makini kama vile Nataka, salasala na La kuchumpa. 

Aidha, Godzilla alijizolea umaarufu na mashabiki wengi kutokana na umahiri wake wa kuimba mashahiri ya papo kwa papo maarufu kama 'Freestyle' ambapo alikuwa akishindana na wenzake kama Nikki mbishi na wakazi. 

Taarifa zilizotoka hospitalini Lugalo zinasema kuwa Golden alikuwa ameshafariki wakati anafikishwa hospitalini hapo huku taarifa hizo zikipingana na zile za ISABELLA ambaye ni mtu wa karibu na familia ya Godzilla aliyesema kuwa Zilla aliwahishwa Zahanati kwanza na baadaye hospitali ya Lugalo na amefia huko. 


  Loading...

No comments: