Msanii wa muziki, Rayvanny ametoa video ya wimbo wake mpya ya ‘TETEMA’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
Wimbo wa ‘TETEMA’ unakuja baada ya wawili hao kuachia kibao chao cha Mwanza ambacho kilizua utata mkubwa na kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kufuatia kutokuwa na maudhui mazuri.