RC Makonda Kumuweka Rumande Harmonize Akikutwa Anatumia Bangi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 1, 2019

RC Makonda Kumuweka Rumande Harmonize Akikutwa Anatumia Bangi


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amesema ameongea na Gavana wa Ghana kumchunguza msanii, Harmonize ambaye yupo nchini humo kama anatumia bangi ili kama ni kweli akirudi amuweke rumande.

Hatua hiyo imekuja baada ya Harmonize ambaye yupo nchini Ghana, kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonyesha akivuta kitu kinachotoa moshi.

"Nimemuona mtu mmoja yuko Ghana kule ule moshi unavyotoka ni kama wa Bangi na tayari nimeshaongea na rafiki angu Gavana wa Ghana pale wanisaidie kumfuatilia Harmonize anatumia Bangi au sigara na kama anatumia bangi akitua hapa ni Lock Up moja kwa moja namna unavyojithaminisha ndivyo serikali itakavyo kuthamini," alisema Makonda.

Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 31,2019  wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Loading...

No comments: