REAL MADRID BADO HAIKO SAWA, YACHARAZWA 2-1 NA GIRONA NYUMBANI BERNABEU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 17, 2019

REAL MADRID BADO HAIKO SAWA, YACHARAZWA 2-1 NA GIRONA NYUMBANI BERNABEUKlabu ya Real Madrid (Los Blancos) wamejikuta wakirudishwa nyuma leo hii katika mbio za ubingwa wa ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama Laliga baada ya kufungwa mabao 2-1 na timu ya GIRONA kutoka jimbo la Katalunya nchini humo. 

Mechi hiyo iliyochezwa mchana wa leo pale uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid ilishuhudia Madrid wakipata bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza dakika ya 25 kupitia kwa kiungo CASEMIRO na kuwafanya watawale vyema kipindi hicho chote mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili ndipo mambo yalipobadilika kwani Girona ambao wanahangaika wasishuke daraja, walikuja na nguvu ya ajabu ya kutaka japo kutoa suluhu mechi hiyo na ndipo walipopata penati dakika ya 64 na dakika ya 65 straika wao Muargentina Christian Stuani akafunga bao la kusawazisha kupitia penati hiyo. 

Wakati Madrid wakihaha namna ya kushinda mechi hiyo na kujiachia, ndipo mshambuliaji wa Girona aitwaye Portu alipopeleka msiba kwa Mashabiki wa Madrid mnamo dakika ya 75 kwa kufunga goli safi kabisa. 


Mnamo dakika ya 90 nahodha wa klabu hiyo ya Madrid, beki Mtukutu Sergio Ramos alitolewa nje kwa kadi nyekundu. 

Mpaka mchezo unaisha, Madrid 1-2 Girona. Matokeo haya yanawafanya Real Madrid wabaki na point 45 na waachwe point 9 na vinara FC BARCELONA huku Atletico Madrid wakirudi nafasi ya 2 baada ya jana kushinda na kufikisha point 47 ambazo ni point 7 pungufu ya vinara Barcelona wenye point 54. 

Takwimu za mchezo huo

Msimamo wa ligi LALIGA
 
Loading...

No comments: