RIO FERDINAND ANENA HAYA BAADA YA UNITED KUPOTEZA DHIDI YA PSG - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 13, 2019

RIO FERDINAND ANENA HAYA BAADA YA UNITED KUPOTEZA DHIDI YA PSGBeki nguli mstaafu wa klabu ya Manchester United RIO FERDINAND amewaasa timu yake ya zamani Man United kufikiria zaidi katika kumaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya jana kuwekewa kikwazo kikubwa sana katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya (Uefa Champions League).

Ili wapite katika hatua hii ya mtoano, Man United wanapaswa kushinda zaidi ya magoli 3-0 jijini Paris katika mechi ya marudiano wiki chache zijazo huku wakiwa katika hali ngumu kwani watawakosa mshambuliaji wao Jesse Lingard (majeruhi) na kiungo aliye katika ubora wa hali ya juu kwa sasa PAul Pogba aliyepewa kadi nyekundu hapo jana. 
Rio anaamini kutokuwepo kwa Pogba katika mchezo huo wa marudiano kumepigilia msumari katika jeneza lao katika mashindano hayo. 

Akiongea na BT Sport Rio alisema: "Wanapaswa kuendelea mbele na kufikiria namna ya kumaliza katika nafasi nne za juu katika ligi kwa sasa. Huu mpambano umekwisha baada ya ile kadi nyekundu kutolewa"

Pogba amekuwa mwenye furaha na akionyesha uwezo na kiwango kikubwa sana tangu ujio wa kocha mpya wa muda Ole-Gunna Solskjaer na hakuna shaka kuwa Man United watahaha kuziba pengo lake katika mechi hiyo ya marudiano mnamo Mwezi March. 

Rio aliongeza: "Watamkosa katika Champions League lakini wana Ligi kuu ambapo atacheza kama kawaida na atapata nafasi ya kuendelea kuonyesha uwezo wake mkubwa."Loading...

No comments: