RTO DELELI AHIMIZA UNYWAJI KIISTARABU KWA MADEREVA MKOANI MOROGORO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 24, 2019

RTO DELELI AHIMIZA UNYWAJI KIISTARABU KWA MADEREVA MKOANI MOROGORO

         Mkuu wa  Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Unywaji kiistaarabu ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha” mkoani humo.

23 Februari 2019,Morogoro.Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imeendelea na kampeni yake ya uelimishaji juu ya unywaji kiistarabu inayolenga kuwafikia wanafunzi wa vyuo,madereva, waendesha vyombo vya umma, na madereva bodaboda mkoani Morogoro.

Kampeni hiyo ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto” itakayofanyika siku ya Jumamosi imelenga kuwafikia watu 1000 kupitia maeneo mbalimbali ikiwamo sehemu za starehe ‘baa’, vyuo pamoja na watumiaji wengine wa barabara mkoani hapo.

Kampeni hiyo imezinduliwa jana Februari 23, 2019 katika Hoteli ya Nashera ambapo wadau mbalimbali wa usafirishaji ikiwamo Jeshi la Polisi, Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) na madereva walishiriki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkurugeni wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha kampeni hiyo imelenga kuwafikia watu 1,000 wakazi wa Mkoa huo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupunguza kiwango cha ajali za barabarani hapa nchini.

Mkurugenzi huyo alisema kampuni hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwmao Jeshi la Polisi-kitengo cha Usalama Barabarani ambapo kampeni hiyo imekwisha kufanyika katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam mapema mwaka huu.

“Katika kampeni hii tunatoa vifaa mbalimbali vya uelimishaji ikiwamo vipeperushi, vibandiko (stika), makoti ya usalama (reflectors), fulana pamoja na kuwashirikisha wadau katika majadiliano yanayolenga katika kutokomeza baadhi ya mila na desturi potofu juu ya matumizi ya pombe,” alisema Wanyancha.

Aliongezaa “Unywaji kistaarabu hauishii tu katika kupunguza kiwango cha pombe bali ni kutokuruhusu pombe itawale maisha yako au iongoze mahusiano yako.”
    Mkuu wa  Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli akionyesha mfano wa makoti ya usalama barabarani (Reflectors) kwaajili ya madereva bodaboda mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Unywaji kiistaarabu ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha” inayoratibiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL).Kampeni hiyo inalenga kupunguza idadi ya ajali zitokanazo na ulevi hapa nchini

Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabrani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli aliishukuru SBL kwa jitihada hizo na kwamba kwa kulishirika Jeshi la Polisi ni chachu ya kuleta mabadiliko chanya na kuzifanya barabara kuwa salama  kwa watumiaji.

Hatahivyo, Deleli alisema anasikitishwa na vitendo vya baadhi ya madereva kunywa pombe kiholela pasipo kujali matokeo yake huku akitoa wito kuwa tabia hizo zinatakwa kukoma ili kupunguza ajali zinazowza kuepukika.

Takwimu za ajali nyingi hasa zinazotokea usiku zinasaabishwa na ulevi ambapo sisi ambao ni watumaji wa vilevi tunashauri kuwa unakuwa na dereva ili akusaidie kukurudisha nyumbani kwako maana bila kufanya hivyo tegemea kupata ajali,” alisema Deleli

Aliongeza, “Nafarijika kuona kwamba licha kuwa ni Serengeti ni wazalishaji wa bia lakini wamejitoa kwaajili ya kupambana na tatizo la ulevi hasa kwa maadereva ambao wanabeba dhamana ya maisha ya watu wengi,” alisema Deleli.

Kampeni hiyo imelenga kuwafikia watu 10,000 hapa nchini ili kuwapa elimu ya unywaji kiistarabu ili kupunguza ajali za barabarani.Mkuu wa  Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli akimkabidhi makoti ya usalama barabarani (Reflectors) kwa mmoja wa madereva bodaboda mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Unywaji kiistaarabu ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha” inayoratibiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL).

 


Loading...

No comments: