Salim Aiyee awapasua kichwa Okwi na Kagere - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 22, 2019

Salim Aiyee awapasua kichwa Okwi na Kagere


Mshambuliaji wa Mwadui FC Salim Aiyee, amekua ashikiki kwenye kutupia magoli na hadi sasa ana mabao 12 kwenye ligi akimpoteza mfungaji bora wa msimu uliopita Emmanuel Okwi pamoja na Meddie Kagere wote wa Simba.

Okwi alipewa tuzo ya mfungaji bora msimu wa mwaka 2017/18 bada ya kufunga mabao 20 mpaka sasa ana mabao saba huku akipotezwa na Aiyee.

Aiyee amesema bado ana kazi ngumu ya kufanya kwa sasa kwenye ligi ili kuisaidia timu yake kupata pointi tatu muhimu.

"Nafurahia kuona timu yetu inapata matokeo ni jambo la kujivunia, bado tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha kwamba tunabaki kwenye ligi msimu ujao.

"Ushirikiano ambao ninaupata kutoka kwa wachezaji pamoja na kufuata maelekezo ya mwalimu kunatufanya tupate matokeo, nitafunga kila ninapopata nafasi," amesema Aiyee.

Mwadui FC wanashika nafasi ya nane baada ya kucheza michezo 28 wakiwa wamekusanya pointi 33.
Loading...

No comments: