SBL YAWAKUTANISHA WANAWAKE KUADHIMISHA SIKU YA WAPENDANAO 'VALENTINE'S DAY' - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 14, 2019

SBL YAWAKUTANISHA WANAWAKE KUADHIMISHA SIKU YA WAPENDANAO 'VALENTINE'S DAY'
 Mwenyekiti wa wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL) Anitha Rwehumbiza akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wapendandanao duniani (Valentine’s Day) ambapo SBL imeadhimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kupitia jukwaa liitwalo ‘SBL spirited women’ ili kujadili mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku ya wapendano duniani maarufu kama ‘Valentine’s Day’ Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) imewakutanisha wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Alhamisi Februari 14, 2019 Mwenyekiti wa wanawake wa SBL, Anitha Rwehumbiza amesema lengo kubwa ni kuwainua wanawake ndani na nje ya ofisi kupitia jukwaa maalumu lijulikanalo ‘SBL spirited women’.

Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Chang’ombe jijini hapa pamoja na matawi yaliyopo mikoa ya Mwanza na Moshi.

“Lengo ni kuwainua wanawake katika nyanja tofauti sio tu katika kazi lakini pia nje ya ofisi na  kwa mwaka huu tumeona tujumuike pamoja tuonyeshe upendo wetu kwa wanawake wote wa Serengeti na kuwashukuru wanawake kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuendeleza kiwanda chetu,” amesema Rwehumbiza.

Wafanyakazi wanawake maarufu kama SBL spirited women kutoka mkoani Mwanza wakiwa kwenye vazi la rangi nyekundu wakati wa siku ya wapendanao 'Valentine's Day'


 Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakionyeha Kinywaji maalumu kwaajili ya wanawake kijulikanacho kwa jina la Baileys wakati wa hafla ya kuazimisha siku ya wapendanao ‘Valentine’s Day’ iliyofanyika kwenye Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Chang’ombe jijini hapa. 
Rwehumbiza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL amesema katika siku hiyo ya wapendanao kampuni ya Serengeti inawakumbusha watanzania kuzingatia unywaji kiistaraabu ili kuepusha ajali zitokanazo na ulevi hapa nchini.

“Kwa wateja wetu tunawashukuru sana kwa kuwa pamoja na sisi kwasababu uwepo wetu unategemea zaidi wafanyakazi na vilevile wanywaji wetu wakubwa,” amesema 

Wanawake hao walionyesha umaridadi kwa kuvaa mavazi ya rangi nyekundu ambayo huvaliwa katika siku hiyo na kukabidhiwa kinywaji maalumu kijulikanacho kama ‘Baileys’
kinachotengenezwa na kampuni mama ya Diageo na kusambazwa na kampuni ya bia Serengeti.

Wafanyakazi wa Sereneti Breweries tawi la Moshi wakifurahi wakati wa maadhimisho ya siku ya wapendanao yaliyofanyika leo mkoani hapo

 Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya maadhimisho ya siku ya wapendanao duniani ‘Valentine’s Day’ ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kujadili mchango wao katika ukuaji wa kampuni hiyo.

Loading...

No comments: