SERGIO RAMOS KUHUKUMIWA KWA KUJIPATISHA KADI YA NJANO MAKUSUDI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 27, 2019

SERGIO RAMOS KUHUKUMIWA KWA KUJIPATISHA KADI YA NJANO MAKUSUDI


Nahodha wa klabu ya Real Madrid Sergio Ramos amehukumiwa na shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) kwa kosa la kujipatisha kadi ya njano makusudi katika mechi ya michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya timu ya AJAX ili apumzike mpaka robo fainali.

Beki huyo wa kati alitolewa nje ya uwanja mnamo dakika ya 89 katika mchezo ambao Madrid walishinda 2-1 pale Amsterdam Februari 13 ambapo ilimaanisha kuwa ataukosa mchezo wa marudiano utakaopigwa Santiago Bernabeu hivi karibuni.

Mara baada ya mechi ile kuisha tu, Ramos alikaririwa akisema "atakuwa anadanganya" kama akikataa kuwa alifanya makusudi faulo ili aadhibiwe.

Ingawa baadaye kupitia mitandao ya kijamii aliamua kueleza kwa kukana kuwa halikuwa swala la makusudi, UEFA walianza kufanya uchunguzi wa kimaadili na kukamilisha usiku wa jana jumanne huku ukithibitisha kuwa Ramos alifanya makusudi na anahukumiwa kulingana na ibara ya 15.

Ramos anaweza kupewa adhabu ya kukosa mechi nyingi zaidi pamoja na kupigwa faini kubwa.

sergio ramos
Loading...

No comments: