SERIKALI HAIINGILII MIHIMILI MINGINE YA DOLA: RAIS MAGUFULI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 7, 2019

SERIKALI HAIINGILII MIHIMILI MINGINE YA DOLA: RAIS MAGUFULIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wakati alipowasili kuhudhuria  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk  baada ya kuhudhuria   kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua rasmi gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, , Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Sophia Mjema wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  baada ya kuizindua rasmi akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk, Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird, wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019. Anayetoa maelekezo ni Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalege na Kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea baada ya kulizindua rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Majaji Wakuu Wastaafu Mhe. Augustino ramadhani na Mhe. Mohamed Chande Othmana kabla ya kupiga nao picha ya kumbukumbu kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalegebaada ya kuzindua rasmi Mfumo wa Kielektroniki wa Kuratibu Mashauri (DSDS ll)  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.(PICHA NA IKULU).
NA K-VIS BLOG
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Serikali yake kamwe haiingilii mihimili mingine ya dola. Rais ameyasema hayo leo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2019 wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Sheria.
Rais amesema, kila Muhimili uko huru kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi na wala yeye hana haja ya kuingilia muhimili mwingine.
Rais pia ameipongeza idara ya Mahakama kwa kuboresha utoaji huduma na kwamba ameridhishwa na mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika kipindi kifupi chini ya uiongozi wa Jaji Mkuu, Mhe. Profesa Ibrahim Juma.
Katika maadhimisho hayo, Rais pia amezindua “mahakama inayotembea” Mobile Court Services, na kumtaka Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi, kuitumia mahakama hiyo ili kuharakisha haki za watanzania hususan akina mama wajane ambao wanateseka sana kutokana na mashauri yao kuchukua muda mrefu.
Rais pia ameahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili idara ya Mahakama, na kuwataka majaji na mahakimu kuchapa kazi licha ya changamoto hizo na kwamba Serikali inazitambua na inazifanyia kazi kwa kadiri bajeti inavyoruhusu.
Aidha Rais Magufuli ameinyooshea kidole idara ya upelelezi wa makossa ya jinai kwa kuchukua muda mrefu kuchunguza kesi licha ya kesi zingine kuwa na ushahidi ulio wazi.
Aliwataka mahakimu, majaji na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kufanya kazi bila woga, lakini kwa kumtanguliza Mungu mbele.
 
Loading...

No comments: