Serikali yatangaza kuwatumia wanawake wenye makalio makubwa kama vivutio vya utalii na rasilimali za taifa nchini Uganda - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 8, 2019

Serikali yatangaza kuwatumia wanawake wenye makalio makubwa kama vivutio vya utalii na rasilimali za taifa nchini Uganda

Image result for ‘Miss Curvy Uganda
Waziri wa Utalii nchini Uganda, Godfrey Kiwanda katikati kwenye picha

Serikali nchini Uganda kupitia Wizara ya Utalii nchini humo imetangaza rasmi kuwa itawatumia wanawake wenye maumbo mazuri katika kuvutia watalii nchini humo.

Hayo yametangazwa Juzi Februari 5, 2019 na Waziri wa Utalii nchini humo, Godfrey Kiwanda wakati akizindua shindano la ‘Miss Curvy Uganda’, ambapo amesema wanawake wote watakaoshindana mwaka huu watatumika kama vivutio vya utalii.
Tumejaaliwa kuwa na wanawake wenye maumbo mazuri na ya asili kwanini tusiwatumie kutangaza utalii ile hali wapo nchini mwetu. Tutawatumia wanawake wote watakaofanya vizuri kwenye shindano hili.“amesema Bwana Kiwanda.
Shindano la ‘Miss Curvy’ nchini Uganda limezinduliwa juzi katika hoteli ya Mestil jijini Kampala na tayari wanawake wanaharakati wameanza kupinga mashindano hayo kwa kudai kuwa yanadhalilisha wanawake.
Loading...

No comments: