Spika Ndugai: Simba Imefungwa Goli 5 Sababu Kule Kuna Baridi Sana Inabidi Wakija Kwetu Tucheze Mchana Saa 8 na Jua la Huku Tuwakomeshe na Joto - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 5, 2019

Spika Ndugai: Simba Imefungwa Goli 5 Sababu Kule Kuna Baridi Sana Inabidi Wakija Kwetu Tucheze Mchana Saa 8 na Jua la Huku Tuwakomeshe na Joto


Spika Ndugai: Simba Imefungwa Goli 5 kwasababu Kule Kuna Baridi Sana Inabidi Wakija Kwetu Tucheze Mchana Saa 8 na Jua la Huku Tuwakomeshe na Joto
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kipigo walichokipata Simba nchini Misri, bado kimemuumiza na kuwaumiza Watanzania wengine.

Simba ilikubali kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Al Ahly katika mchezo wa tatu wa Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika Jumamosi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 4, 2019 bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo amewataka Watanzania kuwa wazalendo na timu zao zinapocheza nje ya nchi.

“Asubuhi nilikutana na Mkuchika (Waziri) akawa anaonyesha mkono na kunyoosha vidole vitano, nikakutana na Mwigulu Nchemba naye akawa ananifanyia kama anaendesha bodaboda, nikamuuliza Waziri Mkuu hii maana yake nini, daa ni kipigo cha juzi kweli tulipigwa jamani,” amesema Ndugai na kudai kuwa ilimbid aizime kabisa Tv yake maana hakuweza kuendelea kuangalia.

Spika Ndugai amesema kipigo cha mfululizo kwa timu hiyo kwenye mashindano makubwa ya Ligi ya Mabingwa kinawaumiza wapenzi na mashabiki.

Amewataka wapenzi wa timu nyingine kuunga mkono timu za wenzao wanapocheza na timu za nje ya nchi ili ukifika wakati wote wafanye vizuri.

Hata hivyo aliwatania wabunge kuwa kilichoiponza Simba ni suala zima la baridi ambapo sasa timu ya Al Ahly ikija nchini watalazimika kucheza saa nane mchana ili nao wachezaji wao waumizwe na jua kali.
Loading...

No comments: